Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552610

Siasa of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Tukafufue mchakato wa Katiba ulipoishia" - Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni

Mchakato wa Katiba Mpya Mchakato wa Katiba Mpya

Umoja wa vyama visivyo na uwakilishi Bungeni, umesema hawaoni tija kuanza upya mchakato wa Katiba mpya badala yake mchakato huo uanziae ulipoishia ili kuokoa gharama, ikiwa ni pamoja na kutimiza matakwa ya demokrasia halisi.

Mwenyekiti wa umoja huo Abdul Mluya, amesisitiza malengo yao ya kuonana na Rais Samia na kuvitaka Vyama vingine kutovuruga mipango hiyo kwa maslahi yao binafsi.

"tunadhani huu ni wakati sahihi, twende tukafufue mchakato ulipoishia, tukapigie kura sheria iundwe irudishwe Bungeni, tupigie kura mchakato wa Katiba pendekezwa,kama tutakuwa na madai basi tutayafanyia kazi baadae,lakini tuifanyie kazi hii iliyokula pesa za walala hoi".

Kauli hii imetoka, ikiwa ni baada ya Rais Samia kufanya Mahojiano yaliyohusisha mchakato huo wa Katiba mpya.