Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 27Article 544465

Habari Kuu of Sunday, 27 June 2021

Chanzo: millardayo.com

"Tumeanza mazungumzo kufufua Banadari ya Bagamoyo" Rais Samia

play video"Tumeanza mazungumzo kufufua Banadari ya Bagamoyo" Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa bandari ya Bagamoyo pamoja na kufufua mradi wa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma kwa kuwa soko la chuma kwa Dunia limepanda.

Kauli hiyo ameitoa mkoani Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.

“Kuhusu bandari ya Bagamoyo tumeanza mazungumzo ya kufufua mradi wote ule wa Bagamoyo pamoja na Mchuchuma na Liganga nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika zinaendelea na mazungumzo kuona tatizo ni nini”  Rais Samia

“Kuhusu Mchuchuma na Liganga mazungumza yanaendelea kuona tatizo ni nini serikali inaweza kujitoa mpaka wapi, mwekezaji ajitoe mpaka wapi na taarifa zilizopo Duniani chuma imepanda bei ni wakati mzuri wa kuharakisha na kufanya ule mradi” Rais Samia

DRONE: SIMBA, AZAM BALAA ZITO, ZAZIBA NJIA, TAZAMA UWANAJ ULIVYOJAA