Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552640

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Tumekusanya Bilioni 48 Tozo za miamala"- Mwigulu

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Waziri wa Fedha, Mwigulu nchemba, ametoa ripoti ya mwezi ya tozo mpya za Miamala, na kubainisha kuwa kwa takribani wiki nne tangu kuazishwa kwa tozo hiyo tayari Serikali imekusanya kiasi cha bilioni 48.

Ameeleza kuwa zaidi ya Bilioni 22 ilishapelekwakwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya zaidi ya 90, pia fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Tangu makato ya tozo yaanze kwa hizi Wiki 4 hadi leo tumekusanya zaidi ya Bilioni 48, zaidi ya Bil 22 tulishapeleka kwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya (zaidi ya vituo 90), leo tumepeleka zaidi ya Bil 15 kwenye eneo hilohilo na kufanya vituo kuwa zaidi ya 150“

“Kati ya hizi zaidi ya Tsh.Bil 48 tulizokusanya kwenye makato ya tozo kwa hizi Wiki nne, zaidi ya Bil 7 zimepelekwa kwenye madarasa, mtaona wenyewe tumepeleka fedha zijenge vituo 150 ambavyo vinaokoa maisha yetu, pia madarasa zaidi ya 500, ni Watoto wetu wanasoma”

Waziri huyo amebainisha pia kuhusu makusanyo yaliyofanyika Zanzibarkuwa ni takribani Bilioni 1.6.

“Ndani ya Wiki hizo nne za makato kwenye miamala kwa miezi hii minne kwa upande wa Zanzibar wamekusanya Bilion 1.6, kwahiyo utaona jambo hili lina matokeo"