Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 29Article 544723

Habari Kuu of Tuesday, 29 June 2021

Chanzo: millardayo.com

"Tunataka tujue idadi ya Vijiji&" Waziri Aweso

Wizara ya Maji imesema inafanya mageuzi makubwa kwenye suala la maji na kwamba inataka kujua idadi ya vijiji vyote vilivyopo Tanzania, na kuvibaini vile ambavyo vimekwishapata maji na vile ambavyo havina maji safi na salama kwa lengo la kuhakikisha inaongeza nguvu katika usambazaji.

Kauli hiyo imetolewa leo Juni 29, 2021, na Waziri wa Maji Jumaa Aweso, wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Halima Mdee, aliyehoji mpango wa Wizara hiyo kutumia utaratibu wa sensa ya watu na makazi ili kupata takwimu halisi ya kila nyumba zinazopata maji.

“Wizara yetu ya Maji inafanya mageuzi makubwa sana tumekutana na watu wa takwimu lakini tunataka tujiongeze mbali badala tu ya kusema asilimia ya watu wanaopata maji twende mbali zaidi tunataka tujue Tanzania kuna vijiji vingapi, vingapi vimepata maji na vipi ambavyo havijapata ili tuhakikishe tunaongeza nguvu maeneo ambayo hayana maji huduma ya maji safi na salama,” Waziri Aweso.

KAULI YA MDUDE: NITATEMA NYONGO