Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541231

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: millardayo.com

"Tuweke bucha za nyani na ngedere Wachina wanunue"Mbunge

Mbunge wa Bunda Vijini Mwita Getere, ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii itoe kibali na ifungue mabucha ya nyama ya Ngedere na Nyani kwa ajili ya kuwauzia Wachina kwa kuwa wanyama hao wanazaliana kwa wingi na ni waharibifu wa mazao.

Kauli hiyo imetolewa  Bungeni Dodoma, wakati wabunge wakiendelea kuchangia bajeti ya Wizara ya Maliasili, na ndipo uliopoibuka mjadala wa Ngedere, kushambulia mashamba ya wananchi na kuvuna hususani mahindi kama wameyalima wao.

“Ifike wakati sasa watu wa maliasili waangalie, kama wenzetu hapa wachina hivi vitu vyote wanakula, kwanini hizo bucha za Nyani na Ngedere zisiwepo hapa nchini ili waje wanunue hizo nyama wapelekea huko?”, Mbunge Getere

PROF. JAY AIBUKA NA MAPYA “DIAMOND PLATNUMZ AJIFUNZE, NGUMU SANA, WAPINZANI, MATABAKA”

Join our Newsletter