Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 24Article 573892

Habari Kuu of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

UNESCO Yatangaza Julai 7 Kuwa Siku ya Kiswahili Duniani

Julai 7 Kila Mwaka Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7 Kila Mwaka Siku ya Kiswahili Duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Taarifa hiyo imetangazwa Makao Makuu ya UNESCO mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO azimio maalum la kuitangaza siku hiyo limepitishwa na wanachama wote bila kupungwa, tovuti ya taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza.

Hatua hiyo inakifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kuwa na siku maalum ya kuadhimishwa.

Kiswahili hadi sasa tayari kinatambulika kama miongoni mwa lugha rasmi Umoja wa Afrika, na kinatumika kama lugha rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bunge la Afrika na ni moja ya lugha za Afrika zinazozungumzwa na watu wengi duniani.