Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 14Article 585721

Habari za Afya of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

UNICEF yazituhumu nchi tajiri kutoa misaada ya chanjo zinazokaribia kuisha muda

UNICEF yazituhumu nchi tajiri kutoa misaada ya chanjo zinazokaribia kuisha muda UNICEF yazituhumu nchi tajiri kutoa misaada ya chanjo zinazokaribia kuisha muda

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limesema kasi ya maambukizi ya virusi vya corona aina ya omicron inaanza kupungua barani Afrika, baada ya wiki kadhaa za kusambaa kwa haraka.

Mkurugenzi wa shirika hilo anayehusika na hali ya dharura kiafya barani Afrika, Abdou Salam Gueye amesema Afrika inaondokana na kitisho cha wimbi la nne la covid-19. Aidha, afisa huyo amesema maambukizi yamekuwa yakipanda kwa kasi kwa wiki sita mfululizo lakini sasa kasi hiyo inashuka.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, wimbi hili la nne ndilo lililodumu kwa muda mfupi zaidi barani Afrika. Hata hivyo, ameonya kuwa viwango vya watu waliopokea chanjo Afrika vinabaki kuwa vya chini.

Nchi tajiri zatoa chanjo zinazokaribia kumaliza muda wake

Katika taarifa nyingine, Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef limesema nchi masikini barani Afrika zinataabika kusambaza dozi za chanjo zilizotolewa kama msaada, kabla ya kumalizika muda wake.

Katika taarifa hiyo kwa Bunge la Ulaya, Unicef imesema nchi tajiri zinazigawia nchi masikini chanjo ambazo muda wake wa mwisho kwa matumizi salama unakaribia. Limesema matatizo kwa nchi nyingi masikini yanazidishwa na ukosefu wa vifaa maalumu vya kuzitunza chanjo hizo.

Kwa mujibu wa Unicef, viwango vya chanjo ya msaada vimepanda, lakini utaratibu wa kuzisambaza kwa wahitaji bado unakabiliwa na changamoto.