Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 07Article 555874

Habari Kuu of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

UPDATE: Twitter na Youtube zimerejea kawaida Tanzania, bila VPN

Twitter na Youtube hazipatikani Tanzania bila VPN Twitter na Youtube hazipatikani Tanzania bila VPN

Baada ya kutopatikana hewani kwa masaa takribani matatu, hatimaye mitandao ya Youtube na Twitter imerejea kawaida nchini Tanzania. Hiyo ni baada ya kutokea kupotea hewani kwa mitandao na kusababisha watumiaji wa mitandao hiyo kuwasha VPN ili kuweza kuipata.

Hakujawa na taarifa yoyote kutoka mamlaka za mawasiliano nchini Tanzania ili kuelezea jambo hilo pamoja na kuwepo kwa mijadala kwa watumiaji wa Twitter kuhusu kuzimwa kwa mitandao hiyo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Imeripotiwa kutokea kutopatikana kwa mitandao ya Youtube na Twitter nchini Tanzania kuanzia saa 7 mchana wa September 7, 2021. Ikumbukwe leo ni miaka minne tangu kutokea shambulio la mwanasiasa Tundu Lissu ambaye alikua Mbunge wa CHADEMA nchini humo.

Kutokana na kutopatikana kwa mitandao hiyo kumekua na maoni tofauti kutoka kwa wananchi na watumiaji wa mtandao wa Twitter nchini Tanzania huku wengine wakikumbuka tukio la kufungiwa kwa Twitter miezi kadhaa iliyopita wakati wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.

Wapo waliohusisha jambo hilo na hali ya kisiasa ambapo kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya vyama vya upinzani, serikali na jeshi la polisi.

Haya ni baadhi ya maoni ya wananchi kuhusu kutopatikana kwa mitandao hiyo.