Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552751

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

UPDATES: Mwakabibi Asomewa Mashtaka Mawili

Breaking: Mwakabibi Asomewa Mashtaka Mawili Breaking: Mwakabibi Asomewa Mashtaka Mawili

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Ijumaa, Agosti 20, 2021 imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Manispaa ya Temeke na kubaini kuwepo ubadhilifu wa fedha wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.UPDATES

Aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi na mratibu wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam( DMDP), Edward Haule wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi na jopo la mawakili watatu waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Mshanga Mkunde mbele ye hakimu mkazi mwandamizi, Evodia Kyaruzi.