Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584974

Habari za Afya of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

UTAFITI: Gongo yatajwa kusababisha Saratani ya utumbo

UTAFITI: Gongo yatajwa kusababisha Saratani ya utumbo UTAFITI: Gongo yatajwa kusababisha Saratani ya utumbo

Utafiti uliofanywa na Wanasayansi wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani, IARC umebaini pombe kali ya gongo inayotengenezwa nchini Tanzania, Chang'aa ya Kenya na Kachasu ya Malawi zinasababisha Saratani ya Tumbo hususani kwa Wanaume

Utafiti ulihusisha watu 1,279 waliolazwa wakiugua Saratani ya Tumbo na 1,346 wasiougua Saratani nchini Tanzania, Malawi na Kenya. Walichunguzwa aina za pombe za kienyeji walizotumia

Mwaka 2020 Saratani ya Tumbo ilisababisha vifo vya watu 544,076 duniani. Saratani hiyo ni nadra Afrika Magharibi ilihali imeshamiri Kusini na Mashariki mwa Afrika