Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 560032

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

UTEUZI: Rais Samia kateua wajumbe wa Tume ya Uchaguz NEC

Rais Samia Rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wajumbe wa tatu watakaojaza nafasi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 27, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffari Haniu imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja na Asina Abdillah Omar aliyemaliza muda wake Septemba 15 mwaka huu na sasa ameteuliwa kipindi cha pili kuendelea na majukumu ya NEC.

Wengine ni Magdalena Rwebangira, kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Jaji Jacob Mwambengele wa Mahakama ya Rufani. Uteuzi huo umeanza Septemba 14 mwaka huu.