Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 552007

Siasa of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: eatv.tv

UVCCM walisaidia ushindi wangu- Prof Mkenda

UVCCM walisaidia ushindi wangu- Prof Mkenda UVCCM walisaidia ushindi wangu- Prof Mkenda

Mbunge wa jimbo la Rombo na Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, ameupongeza Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Rombo kwa usimamizi madhubuti wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2020, na kuifanya CCM kuibuka kidedea kwa ushindi wa asilimia nyingi.

Prof Mkenda amesema kuwa Umoja wa Vijana wa CCM ni nguzo imara ya ushindi wa chama hicho kwani katika uchaguzi mkuu walisimamia maslahi ya chama hicho kilichotangazwa mshindi wa uchaguzi.

"Mimi sikuwa na hela za kuwalipa vijana kwa kazi kubwa mliyoifanya wakati wa uchaguzi lakini leo nimewaita kuwashukuru na kuonesha jinsi nilivyotambua umuhimu wenu kwa namna mlivyojitoa kwa maslahi ya jumuiya na chama kwa ujumla wake," amesema Prof Mkenda