Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553357

Habari za Mikoani of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ucheleweshaji malipo ya mkandarasi wasimamisha ujenzi daraja Mto Wami

Daraja jipya la kisasa la Mto Wami Daraja jipya la kisasa la Mto Wami

Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Kisasa la Mto Wami na barabara unganishi unaoendelea kujengwa kwa Fedha za Serikali ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 67.7 umekwishakamilika kwa asilimia 55.6 mpaka sasa na unatarajia kukamilika kabisa ifikapo Septemba mwakani.

Akitoa Taarifa ya Mradi wa Ujenzi huo kwa Bodi ya Mfuko wa Barabara Tanzania iliyofanya ziara ya ukaguzi wa daraja katika eneo hilo la mradi la Mto Wami Mkoani Pwani Mhandisi wa Barabara mradi wa Daraja Jipya la Wami Gabriel Sangusangu amesema mradi huo ambao unagharamiwa na Serikali kwa asilimia mia moja ulitarajiwa kukamilika mwaka huu lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ucheleweshwaji wa malipo kwa mkandarasi hivyo kusababisha mradi huo ukamilike mwakani.

Kwa upande wake M/Kiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Tanzania Joseph Haule amesifu Ujenzi wa Daraja hilo linalojengwa kwa teknolojia ya kisasa na kutoa maagizo kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani kuhakikisha anadhibiti uchimbaji na usombaji wa michanga katika daraja hilo ili kulinda kingo za daraja.