Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 19Article 572713

Siasa of Friday, 19 November 2021

Chanzo: Habarileo

Uhaba wa Dawa wamfikia Katibu Mkuu CCM, ametoa maagizo kwa serikali

Uhaba wa Dawa wamfikia Katibu Mkuu CCM, ametoa maagizo kwa serikali Uhaba wa Dawa wamfikia Katibu Mkuu CCM, ametoa maagizo kwa serikali

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema serikali inakamilisha ujenzi wa viwanda vya dawa ili kumaliza uhaba wa dawa kwenye vituo vya afya na hospitali.

Alisema hayo wilayani Geita katika kikao cha majumuisho ya taarifa za wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili mkoani humo.

Alisema taarifa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Bohari ya Dawa (MSD) zimeeleza hadi sasa viwanda hivyo vinajengwa kwenye maeneo mbalimbali na vingi vimefikia asilimia 80 ya ujenzi na baadhi vimeanza kufanyiwa majaribio.

Chongolo alisema kukamilika kwa ujenzi wa viwanda hivyo kutapunguza gharama za kuagiza dawa nje ya nchi kutoka Sh bilioni 54 kwa mwaka hadi Sh bilioni 23. “Teknolojia inayotengeneza dawa hizo tuna uwezo wa kuihamisha kuileta Tanzania tukazalisha kwa bei ndogo zaidi, viwanda vipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi.”

“Tukienda vizuri, kwa miaka minne au mitano ijayo tutakuwa tunaongelea hadithi ya uhaba wa dawa na dawa zilizokuwa zinauzwa kwa Sh 500 zitauzwa Sh 250 na tutakuwa tumekata gharama kwa nusu,” alisema.

Aidha, Chongolo aliwaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha za miradi ya elimu na afya zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ili itakapokamilika iweze kuakisi thamani ya fedha zilizotumika.