Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 21Article 573259

Habari za Mikoani of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: mwananchidigital

Ujenzi daraja linalounganisha Bulinga, Bwasi wakamilika

Ujenzi daraja linalounganisha Bulinga, Bwasi wakamilika Ujenzi daraja linalounganisha Bulinga, Bwasi wakamilika

Selikali imekamilisha ujenzi wa daraja la Mto Nyamwifi linalounganisha kata za Bulinga na Bwasi katika Halmashauri ya Musoma mkoani Mara baada ya mawasiliano katika eneo hilo kukatika kwa miaka mitatu.

Kukamilika mwa daraja hilo kunatokana na Serikali kutoa zaidi ya Sh300 milioni kwaajili ya ujenzi huo ulioanza mwezi Julai mwaka huu.

Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini, Hussein Abbasi amesema kuwa kati ya fedha hizo Sh127 milioni zilitumika kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo huku Sh173 zikitumika kwaajili ya kukarabati kipende cha barabra chenye urefu wa kilomita 5.5 pamoja na kalvati.

Amesema kuwa katika bajeti ya mwaka huu halmashauri hiyo imetengewa zaidi ya Sh3.6 bilioni tofauti na Sh560 milioni za mwaka wa fedha ulioisha na kwamba tayari fedha hizo zimeanza kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara.

"Pamoja na changamoto za barabara tulizonazo niwaombe wakazi wa halmashauri hii wawe watulivu kwani mwaka huu wa fedha tumepata fedha nyingi na tayari kazi zimeanza mfano tayari tumefungua barabara ya kutoka hapa Bulinga kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kwangwa kwa urefu wa kilomita 4.5 na kazi zingine zinaendelea kila mahali" amesema

akizungumza baada ya daraja hilo kufunguliwa baadhi ya wananchi wa kata hizo wamesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni suluhisho la kudumu kwa changamoto walizokuwa wakikutana nazo hasa nyakati za mvua.

"Wakati wa mvua tulikuwa tukilazimika kuvuka kwa kulipa fedha kutoka kwa watu waliokuwa wakijitolea kutoa huduma ya kuvusha watu jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa usalama wetu na wakati mwingine tulikuwa tunalazimika kuvua nguo ili kuvuka ng'ambo ya pili" amesema Rapahel Magesa

Jonas Malima amesema kuwa mbali na huduma za kijamii lakini pia daraja hilo litakuwa ni kichocheo cha kukua kwa uchumi wa wakazi wa kata hizo huku akisema kuwa hivi sasa wafanyabiashara watakuwa na uwezo wa kufuata bidhaa zao moja kwa moja kutoka mkoani Mwanza kutokana na kuwepo kwa usafiri wa uhakika.