Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540373

Habari Kuu of Friday, 28 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Ujenzi kituo cha utoaji haki wafika asilimia 85

Ujenzi kituo cha utoaji haki wafika asilimia 85 Ujenzi kituo cha utoaji haki wafika asilimia 85

Ujenzi wa Kituo hicho unaotekelezwa na Makandarasi Hainan International LTD, utekelezaji wake ulianza Januari 22 mwaka jana hadi kukamilika unagharimu sh billion 9.2.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Fabian Kwagilwa wakati wa ziara ya kutembelea Kituo hiko kinachoendelea na ujenzi wake kama moja ya utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama,ambao unaendana na mpango wa maendeleo ya Miundombinu.

Mhandisi Kwagilwa amesema ujenzi wa kituo hiko umezingatia mambo muhimu kadhaa kwa ajili ya usalama wa watu watakaoingia kupata huduma za kihaki pamoja na watoaji huduma za haki kimahakama.

Mhandisi huyo aliyataja mambo ambayo yamezingatiwa ni pamoja mazingira bora ya kisasa na rafiki katika utekelezaji wa shughuli za Kimahakama,ikiwemo mifumo mbalimbali inayotumia teknolojia ya kisasa.    

Join our Newsletter