Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557470

Habari Kuu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ujenzi wa Ikulu Dom wafikia 75%

Ujenzi wa Ikulu Dom wafikia  75% Ujenzi wa Ikulu Dom wafikia 75%

MAENDELEO ya ujenzi wa Ikulu Chamwino jijini Dodoma umefikia asilimia 75 huku mkataba wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kisasa ukisainiwa.

Hayo yamesemwa leo na Rais Samia Suluhu, leo katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

“Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa ikulu mpya na sasa umefikia asilimia 75.” amesema na kuongeza

“Ujenzi wa kiwanja kikubwa cha ndege cha kimaitaifa utaanza hivi karibuni kwani jana mkataba wa ujenzi huo umesainiwa.

Aidha alisema ujenzi wa majengo mji wa kiserikali kule Mtumba unaendelea na kwamba kutajengwa majengo makubwa ya ghorofa kutegemea na pesa ambazo kila wizara itapewa.

Amesama tayari serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya mzunguko ambayo ujenzi wake ulicheleweshwa kwa sababu ya taratibu za fidia lakini sasa muda si mrefu utaanza