Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 26Article 574129

Habari za Mikoani of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ukarabati barabara Dodoma kugharimu mabilioni ya fedha

Ukarabati barabara Dodoma kugharimu mabilioni ya fedha Ukarabati barabara Dodoma kugharimu mabilioni ya fedha

Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dodoma, umesema miradi ya kukarabati barabara mkoani humo itagharimu Sh bilioni 48.97. Meneja wa Tarura Mkoa wa Dodoma, Lusako Kilembe alisema Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuna matengenezo ya barabara ya Kisasa, Itega, Njedengwa na Dodoma town, uzibaji wa viraka na kuweka alama za barabarani ambayo kwa ujumla yatagharimu Sh bilioni 193.492.

Kilembe alisema hayo jijini Dodoma katika hafla ya kusaini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara. Alisema pia kuna matengenezo ya barabara katika maeneo ya Ndejengwa na Itega kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi na alisema wametenga Sh milioni 58.9 kwa ajili ya matengenezo hayo.

Kilembe alisema kwa Bahi zimetengwa Sh milioni 948.264 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Mwitikira na Mtitaa kwa kiwango cha changarawe. Alisema katika Halmashauri ya Chamwino kutakuwa na miradi mitatu ya kutengeneza barabara yenye thamani ya Sh bilioni 3.36.

Kongwa itakuwa na miradi yenye thamani ya Sh bilioni 2.09 itakayotekelezwa na kuna miradi ya kutengeneza barabara kwa nguvu kazi thamani yake ni Sh milioni 40 pamoja na matengenezo ya kawaida Mtanana, Makawa kwa kutumia vikundi maalumu.

Meneja wa Tarura Wilaya ya Mpwapwa, Emanuel Lukumay alisema wamesaini mkataba wa Sh bilioni mbili kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami kilometa moja Kibakwe na moja Mpwapwa Mjini na ujenzi wa vivuko na barabara za changarawe.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka aliwataka wakandarasi waliopewa miradi ya barabara katika mkoa huo waifanye kwa kiwango kizuri. “Nawaambia wakandarasi hii bajeti tuliyo nayo hapa ni ya mikoa mitano mkandarasi kaa hapa fanya kazi ili upate kazi nyingine.

Juzi nimeenda Donbosco wana eneo pale likifika wakati wa mvua mtihani kule Nkuhungu kuna shule inajengwa wakati wa mvua kuna shida kubwa. Mimi natamani twende kufanya miradi vizuri,” alisema Mtaka na kuongeza: “Tumekuja kwenye jambo jema kusaini sasa inaleta shida sana ninyi mmetualika kwa upendo halafu baada ya miezi mitatu huu upendo unageuka na kuwa chuki, kesho Takukuru anageuka anawaweka ndani jambo hili linaniumiza.”