Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559405

Habari Kuu of Friday, 24 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ukraine kuanza kutoa Visa nchini

Ukraine kuanza kutoa Visa nchini Ukraine kuanza kutoa Visa nchini

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema mwezi ujao Ukraine inatarajia kufungua kituo cha kushughulikia VISA kwa Watanzania wanaosafiri kwenda nchini humo.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alisema kituo hicho kitaondoa usumbufu kwa Watanzania wanaokwenda nchini humo ambao kwa sasa wanalazimika kwenda Nairobi, Kenya kushugulikia VISA.

Mbarouk alisema hayo baada ya kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Senik kwa kwa njia ya Mtandao.

Alisema walijadili mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na namna ya kushirikiana katika biashara na uwekezaji, kilimo, elimu na viwanda.

Mbarouk Senik alisema Ukraine ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwenye kilimo cha ngano ili kuongeza uzalishaji na ubora

Alisema Senik pia alieleza utayari wa Ukraine kusaini makubaliano na Tanzania ya ushirikiano katika sekta ya elimu.

Kwa mujibu wa Mbarouk, siku zijazo Senik anatarajia kuja Tanzania akiwa na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Ukraine.

Julai mwaka huu Tanzania na Ukraine zilitimiza miaka 29 ya uhusiano wa kidiplomasia. Nchi hizo zimeendelea kushirikiana katika biashara na elimu na mathalani idadi ya watalii wanaokuja nchini kutoka Ukraine imeongezeka kutoka 1,352 mwaka 2014 hadi 7,260 mwaka jana.