Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559246

Habari Kuu of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ukraine kufungua kituo cha kutoa VISA nchini

Ukraine kufungua kituo cha kutoa VISA nchini Ukraine kufungua kituo cha kutoa VISA nchini

Ukraine imethibitisha kuwa Oktoba 2021 inatarajia kufungua kituo chake cha kushughulikia VISA za Watanzania wanaosafiri kwenda nchini humo kwa shughuli mbalimbali.

Hatua hii inalenga kuwaondolea usumbufu Watanzania wanaosafiriki kwenda nchini humo ambapo kwa sasa wanalazimika kupitia jijini Nairobi nchini Kenya kushugulikia VISA za safari zao.

Haya yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye mapema leo amefanya mazunguzo kwa njia ya Mtandao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Senik.

Balozi Mbarouk ameongeza kusema kuwa katika mazumgumzo hayo pia wamejadili namna ya kushirikiana katika maeneo ya Bishara na Uwekezaji, Kilimo, Elimu na Viwanda.