Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 25Article 544192

Habari Kuu of Friday, 25 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Ukwepaji wa kodi liwe jambo la aibu - Dkt. Nchemba

Ukwepaji wa kodi liwe jambo la aibu - Dkt. Nchemba Ukwepaji wa kodi liwe jambo la aibu - Dkt. Nchemba

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ipo haja kwa watoto wadogo kuanza kuelimishwa juu ya umuhimu wa kulipa kodi ili watoto wakue wakijua kwamba ukwepaji wa kodi ama upokeaji na utoaji wa rushwa ni jambo la aibu katika familia.

Submitted by Agnes Kibona on Alhamisi , 24th Jun , 2021 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo ameitoa leo Juni 24, 2021, Bungeni Dodoma na kuongeza kuwa taifa litakalojengwa na watu wa aina hiyo litakuwa ni bora zaidi na kwamba jamii ya sasa haijafikia hatua ya watu kuonashida kujihusisha na masuala ya rushwa na na ukwepaji wa kodi.

"Tumeendelea kuongea na wenzetu wa Wizara ya Elimu kwamba tunakijenga vipi kizazi cha nchi yetu tangu wakiwa wadogo waelewe masuala ya wajibu, kodi na kupinga rushwa, watoto wetu tukiwaambia tangu wadogo wakaanza kuona ni aibu kukamatwa kwenye masuala ya kukwepa kodi, tangu wapo shuleni wakaanza kuona ukionekana unakwepa kodi ama rushwa ni jambo la aibu kwenye familia yenu Taifa litakalojengwa na kizazi cha aina hicho ni bora sana," amesema Dkt. Nchemba.