Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 12Article 542389

Habari Kuu of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ummy awa mbogo fedha kutofikishwa kwenye miradi

Ummy awa mbogo fedha kutofikishwa kwenye miradi Ummy awa mbogo fedha kutofikishwa kwenye miradi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amesema amebaini ubadhirifu wa fedha kwenye baadhi ya halmashauri huku fedha kutopelekwa kwenye miradi ya Maendeleo.

Aidha, amesema ofisi yake inaanda mwongozo wa utoaji mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu iwe na tija.

Akizungumza jana na

Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa jijini hapa, Ummy alisema aliomba taarifa hadi Machi mwaka huu akabaini fedha hazijatengwa maeneo mengine, zimetengwa kwenye karatasi hazijapelekwa kutatua kero za wananchi.

“Kwa miezi miwili niliyokaa TAMISEMI fedha zinapigwa kwenye Halmashauri hazipelekwi kwenye mambo yenye tija kwa wananchi, kwenye elimu kipaumbele ni ujenzi wa madarasa shule za msingi na sekondari, sasa unapitishaje bajeti ya halmashauri wana uhaba wa madarasa ya shule za msingi 7,000 huoni hata moja au matano yatakayojengwa na unapiti-

sha bajeti unaleta,”alisema.

Alishangazwa kwenye mipango ya Halmashauri fedha kurundikwa kwenye semina, matamasha badala ya kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo.

“Kuna Halmashauri unakuta miezi tisa imepeleka asilimia nne wakati ilitakiwa kupeleka Sh milioni 10 lakini anapeleka Sh 400,000, unajiuliza hivi kweli kuna Katibu Tawala Msaidizi?,”

Alisema atahakikisha anafumua sekretarieti za mikoa na kumchambua mmoja baada ya mwingine ili kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Alisema halmashauri zilitengeneza mipango na

bajeti ya maendeleo na kuwataka Makatibu hao kuangalia hayo masuala ya maendeleo yanatatua matatizo ya wananchi.

“ Lengo la kikao hiki tunataka fedha zinazokusanywa kwenye Halmashauri zetu zinakwenda kutatua kero za wananchi na si vinginevyo, kama Halmashauri inapata chini ya Sh bilioni tano inatakiwa kutenga asilimia 40 ya maendeleo na kama inapata zaidi ya Sh bilioni tano inatakiwa kutenga asilimia 60 na kupeleka kwenye maendeleo.”

Alisema, “ Fedha kwenye elimu zinaliwa kwa kisingizio cha ukarabati na umaliziaji hapo muwaangalie, anaenda kukarabati kitu gani anaenda kumalizia kitu gani, mi nimewapenda Bahi amepeleka fedha zote za maendeleo zilizotakiwa na miradi inaonekana.”

Kuhusu mikopo, Mwalimu wizara yake inakamilisha mwongozo ambao utabainisha thamani ya mikopo. “Nitauleta kwenu nisingependa kusema kikundi kipewe kiasi gani tuende kujitathmini kwa hali ya mapato tuliyonayo, kikundi kinachopewa fedha kisipungue Sh milioni 10, kwa kikundi chenye wanawake sita angalau watafanya kitu lakini sio kuwapa Sh milioni mbili.”

Michezo

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni