Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552613

Siasa of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Umoja wa yama visivyo na wakilishi Bungeni wamkingia kifua Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan

Umoja wa vyama visivyo na Uwakilishi Bungeni, umemkingia kifua Rais Samia, juu ya sakata la mchakato wa Katiba mpya, kufuatia tuhuma zilizotolewa na vyama vingine vya upinzani kuwa Rais hataki Katiba Mpya.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Abdul Mluya, wamewataka viongozi wengine wa vyama vya siasa kutojikita katika kulalamika kwani tayari wameshapwewa nafasi ya kukutana na Rais ikiwa ni pamoja na kupeleka mapendekezo ya sheria ya vyama vya siasa kwa Msajili Mkuu wa Vyama vya Siasa.

"sina kumbukukumbu kama Rais amesema hataki mchakato wa katiba mpya, Rais amesema tumpe muda ajenge nchi, na sisi hatupingani na hilo, amekaa miezi mitano, hata kama ungekuwa mwana ndoa huwezi kuonesha vision yako ya kesho kwa ndoa iliyokaa kwa miezi mitano, kwa sisi tuliopata nafasi ya kuzungumza kwenye hotuba yake bungeni, tunajua hajanza hata robo ya yale aliyosema, sisi tunamuunga mkono Rais, tutasubiri".