Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559489

Uhalifu & Adhabu of Friday, 24 September 2021

Chanzo: mwananchidigital

Upande wa mashtaka wafunga ushahid kesi ya Mbowe

Upande wa Mashtaka wafunga ushahid kesi ya Mbowe Upande wa Mashtaka wafunga ushahid kesi ya Mbowe

Upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wafunga ushahidi wao baada ya kuwaita mashahidi watatu.

Wamefunga ushahidi wao leo Ijumaa Septemba 24, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo sasa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ndogo ambaye ni mshtakiwa wa pili Adamu Hassan Kasekwa anatarajia kuanza kujitetea.

Kesi hiyo ndogo inahusu uhali wa uchukuaji wa maelezo yake polisi baada ya kukamatwa.

Mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokelewe Mahakamani kama kielelezo cha usahidi wa upande wa mashtaka wakidai kuwa kabla na wakati wa kuyatoa maelezo hayo mshtakiwa huyo aliteswa.

Walidai pia maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda unaoruhusiwa kisheria.