Uko hapa: NyumbaniHabari2021 12 06Article 576562

Habari Kuu of Monday, 6 December 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Urasimu Ardhi wamkera Rais Samia, haya hapa maagizo wizarani

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia, ameongeza msisitizo kwa kuzitaka Wizara ya Uwekezaji na Ardhi kuhakikisha kuwa wanamaliza urasimu wote ikiwa ni pamoja na kushughulikia matatizo yote yaliyopo kwenye upatikanaji wa ardhi.

Ametoa maagizo hayo wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme cha El Sewedy mapema Desemba 06, 2021 jijini Dar es Salaam chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya mita 15,000 za nyaya, transfoma 1500 na mita 100,000 za umeme.

Rais Samia ameitaka Wizara hizo kumaliza changamoto hizo kuu mbili kwani malengo ya Serikali ni kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kupambanua katika masoko ya kimataifa.

"Kuna suala la urasimu na upatikanaji wa ardhi, Mawaziri wote mjipange, tunashukuru kuwa sasa kibali cha uwekezaji kinatoka ndani ya siku tatu, hili la sera na kodi pia tunaendelea kulishughulikia na mambo yanabadilika, lakini malizeni urasimu wote" Amesema Rais Samia.

Ameongeza kusema kuwa Serikli inajikita zaidi katikakuboresha miunombinu ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na barabara, huku ikijibidiisha katika kubadili sera na masuala yote ya kodi sambamba na kuhakikisha kua usalama wa wawekezaji katika kipindi chote unazingatiwa.