Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573484

Habari za Mikoani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Usafi kila jumamosi mwisho wa mwezi- RC Makalla

Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM. Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametangaza rasmi kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi katika mkoa huo.

RC Makalla ameyasema hayo leo Novemba 22, 2021 alipokuwa akizindua Mkakati wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ndani ya jiji hilo ikiwa ni siku chache ya zoezi la kuwapanga wafanyabiashara wadogo (Machinga) kumalizika.

Hata hivyo RC Makalla amesema licha ya kuwa Jumamosi ya mwisho wa mwezi Novemba itakuwa tarehe 27, 2021 amewaelekeza wananchi wa Dar es Salam kuanza rasmi zoezi la usafi ifikapo Desemba 4, 2021 kwakuwa taifa litakuwa likielekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru Desemba 9, 2021.