Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 14Article 585811

Habari Kuu of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Utafiti ufanyike, ni hatari sana - Lema

Godbless Lema Godbless Lema

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema kuwa inabidi ufanyike utafiti wa haraka wa afya ya akili za watu, kufuatia uwepo wa matukio mengi nchini ya watu kujiua, watoto kuua wazazi wao ama wazazi kuua watoto wao.

Rai hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, hii leo Januari 14, 2022.

"Kumekuwepo na matukio mengi ya hatari nchini, watu kujinyonga, watoto kuua wazazi, wazazi kuua watoto pia na ulevi wa kupindukia, kuna hitajika utafiti wa haraka wa afya ya akili za watu, ugumu wa maisha na kupoteza matumaini kumeongeza msongo wa mawazo na uchungu, ni hatari sana, "- ameandika Lema