Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540562

Habari Kuu of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Utoro,mimba za utotoni zakwamisha elimu

Utoro,mimba za utotoni zakwamisha elimu Utoro,mimba za utotoni zakwamisha elimu

UTORO wa wanafunzi, mimba za utotoni na umbali mrefu kutoka shuleni hadi nyumbani ni miongoni mwa changamoto zinazokabili wanafunzi wa shule zilizoko Rorya mkoani Mara.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Elimu nchini TenMet, Ochola Wayoga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu kwa mwaka 2021 litakalofanyika wilayani Rorya mkoani Mara kuanzia Mei 31 hadi Juni 4 mwaka huu.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni uwekezaji katika mifumo ya elimu kwa maendeleo endelevu.

Alisema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuhamasisha umakini endelevu kwa elimu na kuhakikisha elimu bora inatolewa katika wilaya hiyo na kuwaondolea wanafunzi hao changamoto zinazowakabili.

Alitaja sababu nyingine ya maadhimisho wiki ya Elimu ni kutoa ufahamu kwa umma juu ya madai ya haki ya kupata elimu bora na kuhimiza serikali kuzingatia vikundi vingine kama watoto walemavu na wito wa kupata miundombinu ya shule na vifaa na mafunzo kwa walimu na watu wenye ulemavu.

Alisema mkoa wa Mara umechaguliwa na wadau kwa ajili ya kuungana na wananchi ilikuongeza nguvu katika kuhamasisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote.

Kuhusu matokeo ya mitihani katika wilaya hiyo alisema mkoa umekuwa na changamoto za matokeo ya mitihani katika elimu ya msingi na hata ya kidato cha nne.

"Wadau kwa kushirikiana na serikali na Halmashauri ya Rory tunakwenda kuhamasisha wanafunzi, wazazi, waalimu na watumishi katika sekta ya elimu kusimamia ufaulu na uwekezaji katika mifumo ya elimu kwa maendeleo endelevu," alisema.

Aidha alisema watatumia maadhimisho hayo kuhamasisha serikali kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama watoto wenye ulemavu, wito wa upatikanaji wa miundombinu na vifaa vya shule pamoja na mafunzo ya walimu ikiwa ni pamoja na walimu wenye ulemavu.

Mratibu wa Uhakiki wa Ubora kutoka Shirika la Haki Elimu, Dk Ellen Otaru, alihimiza kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya shule na mazingira ya nyumbani wanakotoka wanafunzi hao jambo litakalosaidia pale mtoto atakapopatwa changamoto.

Join our Newsletter