Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 17Article 543064

Habari Kuu of Thursday, 17 June 2021

Chanzo: millardayo.com

VIDEO:Mshtakiwa Seth atoa kauli Mahakamani "Tukutane kwa Mkapa"

VIDEO:Mshtakiwa Seth atoa kauli Mahakamani play videoVIDEO:Mshtakiwa Seth atoa kauli Mahakamani "Tukutane kwa Mkapa"

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya shauri linalomkabili. Akiwa ndani ya chumba cha Mahakama Seth ambaye ameingia makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) alisikika akisema “Tukutane kwa Mkapa”.

Seth aliyasema hayo kabla ya Hakimu kuingia katika chumba cha Mahakama. mbali na Seth na Makandege mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji Fedha, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.