Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 552025

Habari Kuu of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

VIDEO: Rais Samia ameyazungumza haya leo SADC

Rais Samia akihutubia leo kwenye mkutano wa SADC play videoRais Samia akihutubia leo kwenye mkutano wa SADC

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amehutubiwa Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulioanza leo tarehe 17 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Baadhi ya mambo aliyoyazungumza ni haya;

“Naongea hapa nikiwa mwanamke pekee kiongozi mkuu wa nchi SADC. Niwaombe sana kaka zangu kwenye nchi zetu, tuongeze nafasi za wanawake kwenye uongozi na kiuchumi.

“Nimefarijika sana kutoa hotuba yangu ya kwanza ya kujitambulisha nikiwa hapa Malawi kwani kwa Watanzania wengi Malawi ni nyumbani na Wamalawi wengi Tanzania ni nyumbani. Asanteni sana.

“Ukanda wetu wa SADC unasifika kwa hali ya usalama na amani ingawa kuna migogoro midogo midogo na masuala ya demokrasia yanazidi kushamili ikiwemo kubadilishana uongozi mfano mzuri ni kitendo walichoonyesha ndugu zetu Zambia baada ya uchaguzi kumalizika.

“Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ukanda wa SADC hatupaswi kuridhika, bado tunakabiliwa na changamoto nyingi. Jukumu la kutatua changamoto hizo tulizonazo ni letu sisi tuliyopewa dhamana ya kuongoza kwa kushirikiana na wananchi wetu

“Nataka kuwasihi Kaka zangu, wa ukanda huu wa SADC tuendelee kushirikiana katika kuendeleza jitihada za kuwainua na kuwawezesha kiuchumi na kisiasa wanawake kwenye nchi zetu.

“Binafsi nimefarijika kutoa hotuba yangu ya kujitambulisha kwa wakuu wa nchi na serikali nikiwa hapa Malawi, nimefurahi kwa sababu Watanzania wengi Malawi ni nyumbani na kwa wamalawi wengi Tanzania ni nyumbani,”amesema Rais Samia.