Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 573997

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Vigezo na Masharti kwa wanafunzi watakaorejea shule baada ya kupata ujauzito

Vigezo na Masharti kwa wanafunzi watakaorejea shule baada ya kupata ujauzito Vigezo na Masharti kwa wanafunzi watakaorejea shule baada ya kupata ujauzito

Baada ya kuwepo kwa mvutano mkubwa baina ya wadau wa masuala ya elimu kuhusu zuio la kurudi shule kwa wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali lililowahi kuwekwa na hayati Rais Magufuli, hatimaye Serikali imekubali kuondoa zuio hilo na sasa wanafunzi wote wanaweza kurudi kwenye mfumo rasmi wa masomo.

Pamoja na tamko hilo la kuruhusu wanafunzi kurudi shule, serikali imetoa waraka wa elimu ambao unaweka muongozo wa namna jinsi suala hilo litakavyotekelezwa.

Utekelezaji wa Waraka Huu

Ili kutekeleza Waraka huu, wadau mbalimbali wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kama ifuatavyo:

i) Wanafunzi watakaokatiza masomo yao kutokana na ujauzito au utoro wataruhusiwa kurudi shuleni ndani ya miaka miwili tangu walipokatiza masomo yao;

ii) Wakuu wa Shule/Walimu Wakuu wahakikishe wanafunzi waliokatiza masomo na kurudi shuleni wanapata huduma za ushauri na unasihi iii kuwajenga kisaikolojia sambamba na wanafunzi wengine waliopo shuleni;

iii) Wakuu wa Shule/Walimu Wakuu wahakikishe mwanafunzi aliyekatiza masomo anarejea mwanzoni mwa mwaka wa masomo katika darasa alilokuwa anasoma;

iv) Walimu wahakikishe kwamba mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji unafanyika katika mazingira bora kwa wanafunzi wote; na v) Viongozi wa Elimu katika ngazi zote wafuatilie na kutathmini utekelezaji wa Waraka huu.

Mipaka ya Waraka

Waraka huu hautawahusu wanafunzi wanaofukuzwa shule kutokana na makosa yenye mwelekeo wa jinai au mwenendo unaohatarisha amani shuleni. Wanafunzi watakaothibitika kutenda makosa hayo na kufukuzwa shule wanashauriwa kuendelea na masomo kupitia elimu nje ya mfumo rasmi.