Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552139

Habari Kuu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Vigogo Bandari watimuliwa Bungeni

Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(TPA), imewatimua Vigogo wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwenye kikao kisha kuwapa wiki mbili kujipanga upya kujibu hoja za ukaguzi baaada ya kutoridhishwa na majibu waliyotoa.

Mwenyekiti wa Kamti hiyo, Naghenjwa Kaboyoka, amesema TPA ilipata Hati isiyoridhisha katika ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) kutokana na mifumo yao kutokuwa mizuri.

"Mifumo haijakaa vizuri, tumewaambia Ofisi ya CAG watuletee Taarifa za Ukaguzi Maalum uliofanyika ili tufanye maamuzi sahihi"

"Bado inaonesha hawa watu hawajafanya lolote, wanasuasua sana, hata wahasibu wao walionekana hawajui kazi maana hata maswali wanayoulizwa wameshindwa kujibu tumewarudisha warudi tena baada ya siku 14"

Katika Ripoti iliyotolewa na CAG, kwa mwaka 2019/2020 ilionesha vitendo vya ubadhirifu na ukosefu wa ripoti za mapato za siku zitakazo wezesha kuhakiki mapato ya mwezi.