Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 09Article 546190

Dini of Friday, 9 July 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Vigogo EAGT Wapigwa Chini

Vigogo EAGT Wapigwa Chini Vigogo EAGT Wapigwa Chini

Kanisa la The Evengalistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) kupitia kwa Baraza la Wadhamini wa Kanisa hilo limewataja Kadawi Lucas Limbu na Michael Gautu kuwa siyo wahusika tena wa majengo yanayohusika na EAGT yaliyopo kiwanja namba 1 Barabara ya Nyerer Dar.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini EAGT, Askofu Rev Dkt Joshua Benjamini Wawa na kuongeza kuwa kanisa halitahusika kwa lolote juu ya sababu yoyote ya watu hao.

“Kanisa halitahusika kwenye makubaliano yoyote ambayo ndugu Kadawi Lucas Limbu na Michael Gautu watafanya kwa sababu siyo sehemu ya wahusika wa majengo ya EAGT yaliyopo kiwanja namba 1 Barabara ya Nyerere Dar,” alisema askofu Wawa.

Share this:TweetWhatsApp Related