Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 573967

Habari za Mikoani of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Vigogo walafi kubananishwa sakata la machinga Dar

Vigogo walafi kubananishwa sakata la machinga Dar Vigogo walafi kubananishwa sakata la machinga Dar

Zikiwa zimepita zaidi ya siku 20 tangu wamachinga waanze kuondolewa katika maeneo yasiyo rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema endapo watarejea, watakaochukuliwa ni hatua ni watendaji husika.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakuu wa wilaya, watendaji wa kata na mitaa kuingia mikataba na wakurugenzi wa manispaa husika kuhusu utekelezaji wa Kampeni ya Usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Ameongeza kusema kuwa, kuna watu wasio waaminifu wanawaambia wafanyabiashara wawape kiasi fulani cha fedha ili waendelee kufanya shughuli zao maeneo yasiyoruhusiwa.

Juzi, Makalla alizindua kampeni ya kudumu yenye kauli mbiu ya “Pendezesha Dar es Salaam” ikiwa na mkakati wa kuhakikisha wamachinga hawarudi kwenye maeneo waliyoondolewa.

Mkakati huo wa usafi utahusisha mtu mmoja mmoja, taasisi za umma na binafsi huku kila mtu akitakiwa kulinda eneo lake kwa kushirikiana na uongozi wa eneo husika.

Hata hivyo, alisema baada ya kuwaondoa wamachinga sasa mji wa Dar es Salaam unapumua na watu wanatembea kwa uhuru tofauti na ilivyokuwa awali.