Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583939

Habari Kuu of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Vijana tafuteni kazi na si ajira - Rais Samia

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Vijana nchini kujikita zaidi katika kutafuta fursa za kazi badala ya fursa za ajira.

Rais ametoa wito huo wakati wa kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibari huko wilaya ya mkoani Kusini Pemba.

Amesema ni lazima Vijana wakatambua kuwa ajira ambazo zimekuwa zikitangazwa hazitoshi, hivyo ni lazima wakajielekeza katika kufanya kazi ambazo zitawaingizia kipato chao cha kila siku.