Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 09Article 546154

Habari za Mikoani of Friday, 9 July 2021

Chanzo: ippmedia.com

Vijana wakumbushwa kufanya kazi kwa bidii

Mbio za Mwenge Mbio za Mwenge

Wito huo umetolewa mara baada ya makabidhiano ya Mwenge kati ya Wilaya ya Sengerema na Misungwi.

Amesema vijana wachukue fursa ya uwajibikaji,kuongeza bidii, ueledi katika kazi na  kujifunza, pia amewataka wananchi kuchukua tahadhali na kujikinga na  maabukizi ya COVID-19, maabukizi ya Virusi vya Ukimwi na  Maralia ili kujenga Taifa lenye afya.

"Nawaomba Watanzania mjiepushe na  rushwa na kuipinga kwa sababu ni adui wa haki na maendeleo pia mzingatie matumizi ya TEHAMA kwani inamchango mkubwa katika shughuli zote za kukuza kiuchumi ikiwemo ukusanyaji wa kodi na biashara" amesema 

Akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ufugaji kuku elfu 10 (AGROBELG) wenye thamani ya million 500, amesema amevutiwa na uwekezaji huo kwani utaleta tija kwa taifa kwa kutoa ajira kwa vijana wengi hasa waliopo katika eneo hilo pamoja na kuchangia pato la Taifa.

Kwa upande wake Afisa Miradi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Steven Kang'ombe, amesema benki hiyo itaendelea kuwawezesha wafugaji ,wavuvi na wakilimo ili kuwanyanyua kiuchumi huku akiwataka wawekezaji kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Veronica Kessy amesema leo Mbio za Mwenge itatembelea miradi tisa ikiwemo uzinduzi wa upandaji program ya elimu ya kompyuta kwa wanafunzi sekondari Idetemya , uzinduzi wa mradi wa uvunaji na uhifadhi wa maji ,kuweka jiwe la msingi mradi wa ufugaji kuku miradi yote ikiwa na thamani ya Billion 1.5.