Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557395

Habari Kuu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Vitu alivyofanya Waziri Kijaji baada ya kuingia Wizara ya Habari

Waziri wa Habari, Ashatu Kijaji Waziri wa Habari, Ashatu Kijaji

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji ameitaka menejimenti na watumishi kutambua dhumuni kuu la wizara hiyo ni kuwatumikia wananchi.

Dkt. Kijaji amesema hayo katika kikao chake cha kwanza na menejimenti ya wizara katika ofisi za wizara, Dodoma mara baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino.

Amesema kuwa watendaji wana wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kwa sababu umma wa Watanzania una uchu wa kusikia kinachoendelea duniani hivyo kabla ya kufungia chombo chochote cha habari ni vema kutekeleza wajibu kwanza.

“Mifumo yote ya Taifa hili ipo chini ya wizara hii na tumeunganishwa na Sekta ya Habari, twendeni tukahakikishe tunafanya kazi kwa matokeo yanayoonekana,” amesema Waziri huyo.