Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540256

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Vyuo vikuu vyatakiwa kujitofautisha

Vyuo vikuu vyatakiwa kujitofautisha Vyuo vikuu vyatakiwa kujitofautisha

VYUO vikuu vimetakiwa kufanya tafiti zinazotatua changamoto za jamii, vinginevyo vitakuwa havina tofauti na shule au vyuo vya kawaida.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo alitoa rai hiyo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa kufunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Majukumu makubwa ya vyuo vikuu vyote duniani ni kufundisha, kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri kwa jamii, hivyo jukumu la kwanza la kufundisha linafanyika katika taasisi zote za kielimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.”

“Majukumu mawili yaliyobaki ya utafiti na huduma kwa jamii ndio yanaweka tofauti kati ya shule, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Hivyo chuo kikuu ambacho wanataaluma wake hawafanyi tafiti basi kinarudi kwenye lile kundi la kwanza,” alisema.

Dk Akwilapo alisema utafiti hutoa nafasi kwa chuo kujitangaza na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuishawishi serikali na hata soko la ajira kwa maana ya waajiriwa.

“Hivyo wanataaluma natambua kuwa kuna matatizo katika upatikanaji wa fedha za kugharamia tafiti kwani mpaka sasa Mfuko wa Kugharamia Tafiti bado ni mdogo kulinganisha na mahitaji ya vyuo vikuu tulivyonavyo.”

“Fedha zilizopo zimekuwa zikipatikana kwa ushindani mkubwa, wapo wanaozipata lakini ni wazi kuwa ili kuzipata vyuo vinapaswa kuwa na watafiti mahiri wanaoweza kuandika miradi muhimu inayotekelezeka na kutumia lugha ya ushawishi,” alisema.

Naye Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye alisema utafiti na ubunifu husaidia chuo kufahamika duniani na ni kigezo muhimu kinachotumika kupima na kulinganisha ubora wa vyuo vikuu duniani.

“utafiti na ubunifu hutoa nafasi ya ushirikiano baina ya taasisi za elimu ya juu, hivyo kuimarisha uhusiano wa kimataifa.”

“Ni ukweli kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama taasisi ya utafiti hakiwezi kustawi na kuwa sehemu ya jumuiya ya maarifa na ujuzi kama hakifanyi tafiti,” alisema.

Alisema kwa kutambua hilo ndio maana chuo hicho kimeweka msisitizo mkubwa kwenye utafiti

Join our Newsletter