Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 11Article 542245

Habari Kuu of Friday, 11 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

WB yavutiwa utekelezaji mpango wa kaya maskini

WB yavutiwa utekelezaji mpango wa kaya maskini WB yavutiwa utekelezaji mpango wa kaya maskini

Akizungumza juzi alipotembelea wanufaika wa mpango huo jijini hapa, mkurugenzi huyo alisema wataendelea kufanya uhakiki wa wanufaika wa mpango huo kwa kutumia vishikwambi.

Alisema wameona njia hiyo ya kutumia vishikwambi imeleta mafanikio kwa kupata walengwa sahihi wa mpango.

Mkurugenzi huyo alisema tayari ameshafanya ziara katika nchi za Afria za Sudan Kaskazini, Sudan Kusini, Tanzania na baadaye atakwenda Kenya.

Dk. Nyamadzabo alisema Tanzania imeonyesha mwelekeo mzuri katika utekelezaji wa mpango huo kwa sababu walengwa wengi wameonyesha kujikwamua kiuchumi.

Alifafanua kuwa malengo makuu ya Benki ya Dunia ni kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo na Tanzania inaendelea kufanikiwa katika masuala hayo.

“Naipongeza Tanzania kwa kutekeleza vizuri utekelezaji wa mpango huu wa TASAF kwa sababu walengwa wengi hivi sasa wameandikishwa shulewatoto kwa asilimia 98 tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Dk. Nyamadzabo.

Aliongeza: “Tutaendelea kufanya tathmini kuona namna gani itakuwa rahisi zaidi ya utekelezaji wa mpango huu wa TASAF ili tuangalie namna ya kuboresha zaidi.”

Aliipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ushirikiano inaouonyesha katika utekelezaji wa TASAF, jambo ambalo linatia moyo kwa watekelezaji wa mpango huo.

Alisema mafanikio mengine ambayo yanaonekana ni watu wanapewa nafasi ya kutafsiri hali waliokuwa nayo awali na wengi wanaonyesha kupandakiuchumi na kuhitaji kuondolewa katika mpango huo.

Akizungumzia upande wa afya, alisema wanufaika wa mpango huo wanaonyesha afya zao kuimarika kwa sababu wanakula milo mitatu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga, alisema zaidi ya vijiji 10,000 vimeweza kufikiwa na TASAF unaotekelezwa kwa ajili ya kuwanusuru watu hao.

Alisema moja ya mafanikio mengine ambayo yamepatikana ni wanafunzi milioni 1.6 waliokuwa hawawezi kujiunga na elimu, lakini hivi sasa wanauwezo huo kutokana na kuwa na uhakika wa kupata milo mitatu.

Alisema awamu ya tatu ya mpango wa TASAF sehemu ya pili itaendelea kutekelezwa mpaka 2024, na kuwataka walengwa wote kuendelea kutambua kuwa mpango huo unaelekea ukingoni na wanapaswa kubuni vitu ambavyo vitaendelea kuwainua kiuchumi.

Naye mnufaika wa mpango huo, Winfrida Mbago, aliishukuru serikali kwa kuleta mpango huo kwa sababu umewasaidia watu wengi kujiinua kiuchumi kutokana na kuwekeza fedha ambazo wanapewa na TASAF.

Join our Newsletter