Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583909

Habari za Afya of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

WHO: Omicron inaua ni hatari

WHO: Kirusi cha Omicron hakipaswi kuainishwa kama hakina makali, kinaua watu WHO: Kirusi cha Omicron hakipaswi kuainishwa kama hakina makali, kinaua watu

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Visa Milioni 9.5 vimeripotiwa ulimwenguni Wiki iliyopita, ikiwa ni ongezeko la 71%.

Japokuwa Kirusi cha Omicron kimeonekana kutosababisha makali kama Delta, WHO imesema Kirusi hicho hakipaswi kuainishwa kama 'Hakina makali'.

Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kama ilivyokuwa kwa aina zilizopita, Omicron inapelekea watu kulazwa na inaua. Pia, kasi ya idadi kubwa ya maambukizi inapelekea Mifumo ya Afya kuzidiwa.