Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552358

Habari za Afya of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: millardAyo

WHO yatoa Baiskeli 100 kwa watoa huduma za afya Kigoma

Dkt Jailos Hiriza, akikabidhi Baiskeli 100 kwa Mganga mkuu mkoani Kigoma Dkt Jailos Hiriza, akikabidhi Baiskeli 100 kwa Mganga mkuu mkoani Kigoma

Shirika la afya Duniani WHO limetoa msaada wa baiskeli 100 mkoani Kigoma kwa ajili ya Wahudumu wa afya ngazi ya jamii waliopo katika maeneo ya mipakani na katika kambi za Wakimbizi ili kuimarisha ufuatilia wa magonjwa ya mlipuko.

Akikabidhi baiskeli hizo kwa Mganga mkuu mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi million 27.7 kupitia mradi wa pamoja wa Kigoma Dkt Jailos Hiriza kutoka ofisi ya WHO Kigoma amesema baiskeli hizo zitakwenda katika Wilaya zote nane ili kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Amesema wamelenga kupeleka baiskeli hizo katika maeneo ya mipakani pamoja na kambi za Wakimbizi kutokana na umuhimu wa maeneo hayo ambayo yamekuwa ni rahisi kupenyeza magonjwa ya mlipuko na kusambaa katika jamii.

Sekta ya afya Kigoma inakiri uwepo wa baiskeli hizo utasaidia Wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa kuwasadia kufika maeneo ya mbali ambayo yalikuwa ni changamoto katika kufikisha elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Covid 19 na mingineyo ambayo yamezikumba baadhi ya nchi zinazopakana na mkoa wa Kigoma.