Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 22Article 559084

Habari Kuu of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: mwananchidigital

WWF kutoa shilingi milioni 200 ujenzi wa mabwawa hifadhi ya Mkomazi

WWF kutoa Shilingi milioni 200 ujenzi wa mabwawa hifadhi ya Mkomazi WWF kutoa Shilingi milioni 200 ujenzi wa mabwawa hifadhi ya Mkomazi

Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) limetoa Sh200 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa mawili pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Mkomazi mkoani Kilimanjaro.

Kati ya mabwawa hayo, moja litajengwa wilayani Same na jingine litajengwa wilayani Mwanga.

Akizungumza katika kilele cha siku ya Faru duniani leo Septemba 22, 2021 wilayani hapa, Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Profesa Noah Sitati amesema wamekuwa wakifanya utafiti wa wanyama pori hasa aina ya Faru, ulioonyesha kuwa wanyama hao wako mbioni kutoweka duniani kama hatua za makusudi zisipochukuliwa.

Profesa Sitati amesema wamejipanga kwakushirikiana na Shirika la uhifadhi Tanzania Tanapa ili kuhakikisha Faru wanaendelea kuwepo na kuongezeka

Profesa Noah amesema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa kwenye maeneo ya hifadhi ni tatizo la maji hivyo wamejipanga kuhakikisha wanasaidia jamii kuondokana na changamoto ya tembo.

"Katika maadhimisho haya tumeona changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni kupungua kwa Faru hasa katika hifadhi zetu. Sambamba na hilo pia kuna changamoto ya tembo wanaoingia kwenye makazi ya wananchi. Hayo yote sisi WWF Tanzania tumejipanga kukabiliana navyo," amesema Profesa Noah.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo akizungumza katika maadhimisho hayo, amesema Serikali itaendelea kusimamia hifadhi za Taifa na kukutangaza utalii ikiwa ni pamoja na kukabiliana na majangili wote kwa wanyama pori.

Naye Naibu Kamishna Kanda ya Kaskazini wa Tanapa, Herman Batiho amesema wameendelea kuchukua hatua mbalimbali za kumlinda Faru kwenye hifadhi hizo, ikiwa ni pamoja na kuwawekea uzio maalum wanyama hao.