Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584920

Habari Kuu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Waandishi wa Habari Waliofariki Katika Ajali ya Gari Simiyu

Waandishi wa Habari Waliofariki Katika Ajali ya Gari Simiyu Waandishi wa Habari Waliofariki Katika Ajali ya Gari Simiyu

Taarifa kamili juu ya ajali iliyohusisha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza. ............................................ Ndugu waandishi wa habari na wadau wa habari , asubuhi ya leo tuliwataarifu taarifa ya awali juu ya ajali ya waandishi wenzetu wa Mkoa wa Mwanza.

Baada ya kufika kwenye Zahanati ya Busenga nilipewa jukumu la kuwataambua marehemu.

Waliofariki ni 1.Husna Milanzi - ITV 2.Johari Shani - Uhuru Digital 3.Antony Chuwa - Freelancer 4.Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza 5.Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi. 1.Tunu Heman - Freelancer 2 Vany Charles - Icon TV

Kwa sasa tupo njiani na miili ya wapendwa wetu kuelekea hospitali ya Mkoa ya Seketoure Mwanza.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Simiyu chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa magari yote mawili na amethibitisha vifo hivyo.

Taarifa nyingine za uratibu wasibu wa msiba tutawajuza.

Mwanza press club tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu.

Kazi ya Bwana haina makosa, jina lake lihidimiwe.

Edwin Soko Mwenyekiti Mwanza Press Club 11.01.2022