Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 11Article 542194

Habari Kuu of Friday, 11 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wabunge: Bajeti imejibu matatizo ya wanyonge

Wabunge: Bajeti imejibu matatizo ya wanyonge Wabunge: Bajeti imejibu matatizo ya wanyonge

WABUNGE wamesema Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 imejibu matatizo ya watu wa kawaida wakiwemo waendesha bodaboda kwa kupunguza faini hadi Sh 10,000.

Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kuwasilisha bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Baran alisema bajeti nzuri imezingatia mahitaji ya watu wanyonge.

Baran alisema bajeti ni nzuri kwa sababu inataka kuwaondolea kero wananchi wa kawaida wakiwemo wa vijijini kwa kuwajengea barabara.

Pia bajeti hiyo imewakumbuka madiwani kwa serikali kuu kuwalipia posho kwa ajili ya shughuli zao za kuwakilisha wananchi ngazi ya kata.

Mbunge wa Viti Maalumu, Easter Matiko (Chadema) alisema bajeti ni nzuri kuwapunguzia mzigo bodaboda kulipa faini kutoka sh 30,000 hadi 10,000.

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilary (CCM) alisema bajeti imegusa kila kada na mtu mmoja mmoja kwa kuamua kuboresha miundombinu kama barabara, kumalizia ma-

boma ya afya na huduma za maji kwa kuzitafutia fedha.

Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Juma Abdallah (CCM) alisema kitu kizuri katika bajeti ni kuwafikiria bodaboda kwani itasaidia kuboresha huduma zao na kutumia fedha katika maendeleo mengine badala ya kulipia faini.

Join our Newsletter