Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541246

Siasa ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wabunge waonya vibali vya kusafirisha wanyama nje

Wabunge waonya vibali vya kusafirisha wanyama nje Wabunge waonya vibali vya kusafirisha wanyama nje

WABUNGE wameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuacha kutoa vibali vya kusafirisha wanyama nje ya nchi kwa kile walichosema, ipo siku watalii hawatafika nchini kwa sababu watakuwa wanaona wanyama kwenye bustani zao.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo bungeni jana na juzi, walisema, utoaji vibali hivyo hauna tija kwani itapunguza idadi ya watalii kuja nchini.

Mbunge wa Hai, Saasisha Mafuwe (CCM) alisema vibali hivyo vya kusafirisha wanyama hai zitaua ama kupunguza utalii .Wanyama wanaoongoza kwa kuuza nje ya nchi ni simba, vyura na ndege.

Alisema wizara inatakiwa kuangalia suala hilo kutokana na umuhimu wake kwa sekta ya utalii ambayo inachangia asilimia 17.6 katika pato la taifa kati ya asilimia 21 .

Mbunge wa Viti Maalumu, Ngwasi Kamani (CCM) alisema usafirishaji wa viumbe hai kwenda nje ya nchi utaathiri upatikanaji wa fedha za kigeni ambazo zinapatikana kutokana na utalii lakini pia ajira milioni 1.6 zitapungua kutokana na watalii kutokuja nchini.

Alisema wanunuzi hao watakwenda kuzalisha aina bora zaidi za wanyama hao na hivyo kusababisha kuua biashara ya utalii nchini.

Join our Newsletter