Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 09Article 556441

Habari za Afya of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wabunge wataka Usimamizi na Usalama wa Chakula kuwa chini ya Wizara ya Afya

Usimamizi wa Usalama wa Chakula kuwa chini ya Wizara ya Afya Usimamizi wa Usalama wa Chakula kuwa chini ya Wizara ya Afya

Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, limeazimia kufanya mabadiliko ya Usimamizi wa usalama wa chakula kutoka katika Wizara ya Viwanda na Chakula kwenda kwenye Wizara ya Afya.

Wakichangia maoni Wabunge kuhusu jambo hilo ambalo tayari lipo kwenye utekelezaji duniani kote chini ya agizo la Umoja wa Mataifa la kuzitaka nchi zote duniani kuweka usimamizi huo chini ya Wizara ya Afya.

Mbunge wa Viti maalumu kutoka CCM, Neema Lugangira, ametoa maoni kwa kuishauri serikali iweze kuhamisha suala hili ili kuweza kuendana na agizo la Umoja wa Mataifa na kuwa itasaidia katika kumkinga mlaji na changamoto za chakula.

"Tunahitaji Sheria ya Usalama wa Chakula , kwani itaweza kulinda walaji wasipate changamoto ya chakula, na jmabo hili ni jukumu la wizara ya afya" amesema Mbunge huyo.

Ameongeza kusema kuwa anaisisitiza serikali iweze kulitazama suala hilo kwani litasaidia kuendana na agizo la umoja wa Mataifa ili kuiweza nchi kunufaika na mapango wa dunia nzima.

Kwasasa suala la Usimamizi wa chakula lipo kwenye Wizara ya Viwanda na chakula na linasimamiwa na shirikia la viwango la TBS.