Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 26Article 539935

Habari Kuu of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wabunge wataka nyongeza bajeti ya kilimo 

Wabunge wataka nyongeza bajeti ya kilimo  Wabunge wataka nyongeza bajeti ya kilimo 

BUNGE limeishauri serikali itenge bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Kilimo ili kukidhi kutekeleza programu za kuimarisha sekta hiyo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji pia imeishauri serikali iajiri maofisa ugani wa kutosha ili waelimishe wakulima kuhusu namna bora ya kuzalisha mazao.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Athuman Maige aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha maoni na mapendekezo ya kamati hiyo kwa bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Maige alisema kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 sekta ya kilimo imetengewa bajeti chini ya asilimia moja ambayo ni sawa na asilimia 0.08 ya bajeti ya serikali kiasi ambacho ni pungufu ya makubaliano ya Azimio la Maputo na badaaye Malabo linalotaka nchi wanachama kutenga angalau asilimia 10 ya bajeti ya taifa.

Alisema kamati pia inaishauri serikali iajiri maofisa ugani na iwatengee rasilimali fedha, iwape vitendea kazi, na mafunzo ya mara kwa mara.

Maige alisema kamati inashauri serikali iangalie uwezekano wa kutunga sheria itakayozitaka halmashauri za mikoa na wilaya kurudisha sehemu ya tozo zitokanazo na mazao ya kilimo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo.

Kamati ilipongeza juhudi za serikali kuijengea uwezo Wakala wa Mbegu (ASA), lakini itambue kuwa kazi ya uzalishaji wa mbegu bora lazima iendane na utafiti wakala hiyo iongezwe fedha na zitolewe kwa wakati.

Alishauri serikali iwekezze nguvu kubwa kwenye uzalishaji wa mbegu za mafuta ya alizeti, mchikichi na ngano ili kupunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza bidhaa nje ya nchi.

Kamati iliwaeleza wabunge kuwa inatambua juhudi za serikali kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa kwa kujenga vihenge na maghala ya kuhifadhi mazao.

Kamati imeishauri serikali iiwezeshe kifedha Mamlaka ya Barabara Vijijini (TARURA) kwa kupewa fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara zitakazosaidia kutoa mazao ya wakulima shambani.

Iliishauri serikali iweke utaratibu kuwezesha upatikanaji wa mikopo rafiki kwa sekta ya kilimo na kwamba, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) iwe na kitengo cha mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima wadogo

Join our Newsletter