Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 11Article 542266

Habari Kuu of Friday, 11 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Rais Samia atengua uteuzi wa Chalamila, Hapi aahamishwa

Rais Samia atengua uteuzi wa Chalamila, Hapi aahamishwa Rais Samia atengua uteuzi wa Chalamila, Hapi aahamishwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo June 11, 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi. Robert Gabriel Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Albert Chalamila uteuzi wake umetenguliwa

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora

Aidha Ndugu Zuwena Omari Jiri ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae.

LIVE: BAJETI YA BATA, FAINI ZAPUNGUZWA, BIA PUNGUZO, MADIWANI KULIPWA

Michezo

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni