Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 23Article 543958

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 23 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wafanyakazi Watatu wa Letshego Wapandishwa Kisutu

Wafanyakazi Watatu wa Letshego Wapandishwa Kisutu Wafanyakazi Watatu wa Letshego Wapandishwa Kisutu

Wafanyakazi Watatu wa Letshego Wapandishwa Kisutu June 23, 2021 by Denis MtimaWafanyakazi watatu wa Taasisi ya fedha ya Letshego maarufu kama Faidika Limited wakipandishwa mahakamani.Wafanyakazi watatu wa Taasisi ya fedha ya Letshego maarufu kama Faidika Limited, wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la wizi wa Tsh Milioni 700.Akiwasomea hati ya mashtaka wakili wa serikali Faraja Ngukah mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Elisha Tengeni , Donald Kwaya na Elisha Mboka.Wakili Ngukah alidai kati ya Januari mwaka 2016 hadi Septemba mwaka 2017  washitakiwa waliiba sh milioni 700 mali ya Kampuni ya Letshego Tanzania Limited  maarufu kama Faidika fedha ambazo zilifika kwao kutokana na nafasi zao za uwajili.Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha mahakamani fedha taslim au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 350.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Juni 30 mwala huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wote wamepelekwa maabusu.