Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 14Article 546976

Habari za Mikoani of Wednesday, 14 July 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Waganga wa Jadi Wajenga Madarasa

Waganga wa Jadi Wajenga Madarasa Waganga wa Jadi Wajenga Madarasa

Waganga wa Jadi Wajenga Madarasa July 13, 2021 by Global PublishersWAGANGA 87 wa tiba asilia wamefanikiwa kujenga vyumba viwili vya madarasa kwa kutumia fedha zao za uganga, katika Shule ya Sekondari ya Chinameli Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, ili kuunga mkono jitihada za Serikali kuinua kiwango cha elimu wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mkoani humo, Mshauri wa waganga wa Tiba Asilia Mkoa wa Simiyu, Ndabagija Katani alisema kazi ya maendeleo haipaswi kuachwa kwa Serikali peke yake huku akiwashauri waganga wengine nchini kuiga mfano huo.

“Sisi tulianzia kujenga kituo cha polisi, tukashirikiana sisi wataalamu wa tiba asili baadaye tukachimba visima vya shule kwa wanafunzi na tukaona tujenge madarasa mawili hapa, pesa tunazo sisi ni wafugaji wa ngombe tulikuwa tunaleta kila mmoja mifuko miwili,” alisema Katani.

Naye Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga alisema kitendo walichokifanya waganga hao ni cha kushangaza taifa kwani kinaonesha jinsi gani waganga wanauelewa juu ya miradi ya maendeleo na kuwa na muamko katika kuchangia kuinua hususan elimu.

Vyumba hivyo viwili vya madarasa vilivyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Chinameli vilivyogharimu shilingi milioni 29 vimewekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi.

STORI; MWANDISHI WETU

Share this:TweetWhatsApp Related